一 第二十九课 塔图和她的孩子们在家中
来自: 数据分析后生(Just a buffer.)
单词表 Nyumbani 在家 Shuleni 在学校。 Chakula bora 好吃的。 Yai,mayai 鸡蛋。 Maziwa 牛奶。 Mboga 蔬菜 Mchele 米。 Matunda 水果。 -bichi 生的。 -bivu 成熟的。 Kuiva 经过烧煮的,成熟的。 Safi 干净的 -chafu 脏的。 Kukataza 不允许。 Karibu na 靠近……。 Mbali na 远离……。 Ugonjwa 病。 Japo 尽管 Tatu ni mama.Ana watoto watatu:Mashaka,Chausiku,na Sijali.Tatu anakaa shamba pamoja na watoto wake,Ana shamba la matunda na mboga. Tatu anawapa watoto wake chakula bora kila siku.Mboga, mayai, matunda, samaki, viazi, mchele, maziwa na nyama,n.k. Siku moja,Tatu alimwona motto wake Mashaka anakula matunda mabichi, akamkataza. Kwa sababu si mazuri. Tatu alichukua tunda moja zuri akampa Mashaka. Mtoto huyo alifurahi sana, akasema,“Asante mama”. Siku nyingine, Tatu alikwenda mjini pamoja na motto wake, Chausiku. Njiani ,Chausiku alipata kiu,akataka kunywa maji ya mtoni. Mama yake alimkataza, akasema,“maji ya mtoni si safi kwa kunywa, yana vidudu vya magonjwa mbalimbali.” Ngoja tufike nyumbani nitakupa maji safi, japo Chausiku alikuwa na kiu sana, hakunywa maji yale, alingoja mpaka alipofika nyumbani. Tatu anawaeleza watoto wake vizuri;anawafundisha kwa maneno na kwa vitendo pia. Tatu ni mama mwema. 练习37 1. Je,Tatu ana watoto wangapi? Taja majina yao. 2. Je, Tatu anakaa wapi? Anafanya nini? 3. Je,vyakula gani ni bora? 4. Je, nani alikula matunda mabichi? Tatu alifanya nini? 5. je, mtoto alisema nini alipopewa tunda zuri na Tatu? 6. Je, kwa nini Tatu alimkataza Chausiku kunywa maji ya mtoni? 7. Je, Chausiku alifanya nini alipokatazwa kunywa maji na mama yake? 8. Je, Tatu ni mama mwema? Kwa nini unasema hivyo? 9. Je, Tatu alikwenda wapi na Chausiku? 10. Je, maji ya mtoni ni safi kwa kunywa? Kwa nini ? Nyumbani: 有用的短语 Kutandika kitanda, 铺床。 Kupangusa meza 清扫桌子上的灰。 Kuandaa meza 整理桌子。 Fungua mlango, dirisha 开门,窗。 Funga mlango , dirisha 关门, 窗。 Kufua nguo chafu 洗脏衣服。 Kupigapasi nguo 熨衣服。 Kupiga deki 拖地。 Weak chakula mezani 把菜摆上桌。 Kuona njaa, kiu 觉得饿,渴。 Kusafisha vyombo, 洗餐具。 Chuma matunda, 收水果。 Jikoni, 厨房里